Hebrews 1:1-6

Mwana Ni Mkuu Kuliko Malaika

1 aZamani Mwenyezi Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, 2 blakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia kwake aliuumba ulimwengu. 3 cMwana ni mng’ao wa utukufu wa Mwenyezi Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Aliye Mkuu huko mbinguni. 4 dKwa hiyo alifanyika bora kuliko malaika, kama jina alilorithi lilivyo bora kuliko lao.

5 eKwa maana ni malaika yupi ambaye wakati wowote Mwenyezi Mungu alipata kumwambia, “Wewe ni Mwanangu;
leo mimi nimekuzaa?”

Au tena, “Mimi nitakuwa Baba yake,
naye atakuwa Mwanangu?”

6 fTena, Mwenyezi Mungu amletapo mzaliwa wake wa kwanza ulimwenguni, anasema, “Malaika wote wa Mungu na wamsujudu.”

Copyright information for SwhKC